Home » Yatakuwa Sawa by KIBONGE WA YESU

Yatakuwa Sawa by KIBONGE WA YESU

Kwanza nashukuru
Mjini mimi nilifika salama
Tena nashukuru
Maombi yenu yananilinda maana
Kila siku kunapokucha afadhali ya jana
Na maumivu yamenisonga
Kutwa kushika tama
Kuya yangu ya tabu sana
Moyo unapata adhabu
Kodi imekata jana (nadaiwa) eeh
Changamoto, changamoto
Mjini changamoto
Na ile ndoto, yangu ndoto
Imegeuka msoto

Yatakuwa sawa
Kwa ndani ninajipa moyo
Yatakuwa sawa  eeh
Najipiga kifua nasonga mbele
Yatakuwa sawa
Eeh naamini kesho
Yatakuwa sawa
Mungu ananiona ananiona

Hatima kubwa
Lazima ipitie mambo makubwa
Na ndani yangu ninaona ukubwa, wowowowh
Na hakuna kufaulu bila mitihani
Nipe nguvu nizishinde nira za shetani
Sitishwi na vitisho
Mapito ninayopita leo
Kesho yangu ipo
Ninasubiri kitambo kidogo
Mimi ni mwanafunzi nipo darasani ooh
Mungu nifundishe, kutunza imani wowowoh ehe
Changamoto, changamoto
Mjini changamoto
Na ile ndoto, yangu ndoto
Imegeuka msoto

Yatakuwa sawa
Kwa ndani ninajipa moyo
Yatakuwa sawa  eeh
Najipiga kifua nasonga mbele
Yatakuwa sawa
Eeh naamini kesho
Yatakuwa sawa
Mungu ananiona ananiona
Yatakuwa sawa eeeeeh
Yatakuwa sawa
Eeh sichoki kupambana (Yatakuwa sawa)
Usiku na mchana
Namwamini mungu (Yatakuwa sawa)
Kesho yangu itakuwa njema
Eeh eeh
Eeh eeh
Eeh eeh
Eeh eeh