Home » Shuka by IBRAHIM IBRA

Shuka by IBRAHIM IBRA

Aaah oooh oh oh
Baba Shuka, Baba Shuka
Baba Shuka nikuone
Baba Shuka, Baba Shuka
Baba Shuka nikuone

Mimi masikini, masikini wa moyo
Natamani, uje karibu
Nimetembea, nimezunguka, duniani sijaona

Wa kufariji Moyo wangu
Tamanio langu, na ombi langu
Oh baba, Natamani nikuone

Baba Shuka, Baba Shuka
Baba Shuka nikuone
Baba Shuka, Baba Shuka
Baba Shuka nikuone 

Oh Bwana shuka, 
Ni tamanio la moyo wangu Bwana nikuone
Nione ukitenda Mungu
Maana wewe ndiye Mungu mwenye nguvu

Mwenye mamlaka na uweza
Bwana nina imani kuwa unayajua
Na unaenda kubadilisha maisha yetu Mungu
Bwana tunaomba uwepo wako uwe nasi

Tunaomba mkono wako uwe juu yetu Mungu
Tunaomba uponyaji wako Yesu Kristo
Tunaomba urejesho wako mungu
Tunaomba ushuke Yesu

Tunaomba ushushe neema yako
Tunaomba ushushe uponyaji wako
Tunaomba Baba ushushe urejesho wako

Bwana zaidi ya yote tunaomba 
Uonekane maishani mwetu Mungu
Baba ukawe Mungu, ukazidi kuwa Mungu